Duka linalouza zawadi mbalimbali za kiimani kutoka miji takatifu ya Nazareti, Bethlehem, Jerusalem na Roma, zinazofaa kwa sherehe za kidini, matukio mbalimbali ya ki-imani na matumizi binafsi.
Jerusalem Holy Gifts ni duka linalouza zawadi mbalimbali za kiimani kutoka miji takatifu ya Nazareti, Bethlehem, Jerusalem na Roma, zinazofaa kwa sherehe za kidini, matukio mbalimbali ya ki-imani na matumizi binafsi. Bidhaa zetu ni pamoja na mishumaa, rozari, misalaba, picha na mapambo ya ukutani na kidini.
Pia, tuna vitabu mbalimbali vya sala na Ibaada,vya watoto na watu wazima, hivi tunavipata hapa hapa nchini Tanzania. Tunaleta pamoja imani na upendo
katika kila zawadi.
Jerusalem Holy Gifts Ilizaliwa kwa sababu tunaa.. katika kusambaza upendo na kufanya nyakati maalumu kuwa na maana Zaidi (Mith.17:22).
Fikiria, una ubatizo, Komunio ya kwanza,ubarikio ama kipaimara hivi karibuni. Badala ya kuwaza zawadi yoyote tu, sisi tunakuletea zawadi kama rozari, misalaba, vitabu vya ibaada, na zawadi nyingine nyingi za kipekee zinazoendana na matukio haya na vile vile, kusababisha ukuaji wa kiroho.
Tulifikiri, “kwa nini watu wasafiri ama wanasubiri safari ya ndugu, jamaa, na marafiki ili kupata hivi vitu kutoka miji takatifu”. Hapo ndipo hadithi yetu ilipoanza. Tulitaka kua mahali ambapo unaweza kwa urahisi kupata na kutoa hazina za ardhi takatifu bila kusubiri. (Ebr 13:16)
Hivyo tupo, duka lenye nia njema na moyo mkubwa, tayari kujaza nyakati zako upendo na maana. Tufanye sherehe zako na nyakati zako, si tu maalumu, ball takatifu pia.
Karibu Jerusalem Holy Gifts ambapo kila zawadi ya kila tukio ina maana.
Kuwa mahali ambapo watu wanaweza kupata kwa urahisi zawadi za kidini za kweli na maana. Tunataka kuwa chaguo bora na la kwanza kwa ambao wanataka vitu halisi kutoka sehemu za chimbuko la imani (miji takatifu), kwa kuwa na viwango bora na vya juu daima. Tunatumai kua sehemu ya kudumu ya upendo na ukuaji kiroho.
Lengo letu ni kusambaza upendo, huku tukisaidia watu kukua kiimani na kiroho. Tunaleta zawadi halisi za kiimani zinazoleta furaha kutoka ndani ya moyo, zinazo imarisha imani na kuongeza furaha kati ya wapendwa na kwenye matukio ya kidini. Pia kupitia zawadi zetu, Tunaleta historia za kufurahisha kutoka miji takatifu.
Ni sehemu pekee unaweza kupata zawadi/ vitu halisi kutoka miji
mitakatifu, ambayo ni chimbuko la imani ya Kikristo, mbali na kua vitu/zawadi ambazo ni nzuri sana kwa muonekano, Imara sana na pia ni zawadi zenye kugusa fadhila za kiMungu ambazo ni Imani, Matumaini na Upendo.
Jerusalem holy gifts, ni sehemu ambayo mtu akiingia lazima atoke ameguswa kwa namna mbalimbali na kuanzia Mazingira na kila kilichomo. Karibu sana Jerusalem Holy Gifts