Bidhaa zetu ni pamoja na:;
Mishumaa iliyotengenezwa kwa nta ya asali na ya kawaida. Hii imetengenezwa Yerusalem katika kanisa linaloitwa “The holy sepulchre church” hili ni kanisa ambapo vituo vinne vya mwisho vya njia ya msalaba vilitokea.
Misalaba ya aina tofauti. Hii ni misalaba yenye sanamu za Yesu, na isiyokua na sanamu za Yesu, na Misalaba ya njia ya msalaba (hii inaonesha vituo 14 vya njia ya msalaba). Misalaba yote hii imetengenezwa kwa mbao imara sana ya mzeituni. Haiharibiwi na wadudu wala unyevu wala kuvunjika kwa urahisi.
Maji ya baraka kutoka mto Yordani. Mto Yordani ni mto ambao Yohane mbatizaji, allmbatiza Yesu Kristo. Maji haya yanaaminika kua na baraka, hivo tumeyaleta karibu kabisa kwa ajili ya wote waaminio.
Unga wa “Milk Grotto rock powder” huu ni unga unaopatikana sehemu ambayo Maria alimnyonyesha mtoto Yesu. Unga huu huaminika kusaidia uzazi na akina mama wanao nyonyesha. Unga huu hupatikana Bethlehem.